Dar-es-salaam--Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi zaidi ya 40 kutoka duniani kote wanaoudhuria mkutano wa dunia wa kiuchumi, yani World Economic Forum, huko nchini Uswiz katika mji wa Davos.
Kati ya mada kuu zinazotegemewa katika mkutano huu unaoanza kesho, Jumatano, ni mapendekezo juu ya nini kifanyike kutokomeza magonjwa ya saratani duniani kote.
''Shirikisho la wataalamu wa magonjwa ya saratani linaloitwa World Oncology Forum, lenye makao yake makuu nchini Marekani,wamekuwa msitari wa mbele katika kuipenyeza mada hii kuhusu saratani kwenye agenda za mkutano mkuu wa kiuchumi wamwaka huu''
Viongozi wanategemewa kukubaliana juu ya suluhu ya janga la saratani ulimwenguni kote, lakini hasa katika nchi zinazoendelea ambako saratani huwakumba watu wengi kutokana na kukosa elimu ya kutosha juu ya saratani na pia ukosefu wa vipimo bora vya kutambua ugonjwa huu ukiwa bado katika hatua za mwanzo.
Kwa taarifa zaidi tazama ukurasa huu katika wavuti: http://www.thecitizen.co.tz/News/Call-to-step-up-cancer-response/-/1840392/2594102/-/b3hq2jz/-/index.html
Imeripotiwa na Syriacus Buguzi, katika gazeti la The Citizen, kwa msaada wa mashirika ya habari za kisayansi Ulimwenguni, Eureka Alerts.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni